Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) Bw.   Charles Senkondo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika kumbi  za Wakala wakati wa kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Bw. Senkondo aliainisha uwezo wa Wakala kama nyenzo ya kujenga uwezo kwa Wanawake kwa zaidi ya miaka 17 sasa ikitoa fursa za kushiriki katika mafunzo, midahalo na kuongeza ufanisi katika utendaji kwa kutumia teknolojia ya mikutano kwa njia ya video na maabara za Kompyuta.  Alieleza kuwa teknolojia hizi zinawezesha Wanawake kuepuka adha ya kuachana na familia zao ili kusafiri mbali au nje ya nchi, kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na mabingwa waliobobea duniani kwa gharama nafuu.

Pia alieleza kuwa kwa kutumia mtandao wa Wakala imewezekana  kuwashirikisha wanawake wengi zaidi katika maamuzi na kuboresha weledi katika uongozi.

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (VBU) inajipanga kuanzisha Zahanati za Biashara nchini. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Injinia Stella Manyanya wakati wa ufunguzi wa mfululizo wa vikao vya kazi (kwa njia ya Video) kati ya Wizara ya VBU, taasisi zilizopo chini ya Wizara ya VBU na Sekretarieti za Mikoa.

Akifafanua kuhusu Zahanati za Viwanda, Mh. Injinia Manyanya alisema biashara na uwekezaji, kama walivyo binadamu, zinahidaji kuwa na afya ili viweze kuwa na “afya” na kuleta matokeo yaliyotarajiwa. Hivyo Serikali kupitia Wizara, imedhamiria kuona biashara na viwanda vilivyoanzishwa havifi ili kutimiza azma ya Serikali kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Wakati wa Vikao hivyo, Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliwasilisha mada kuhusu Milki Ubunifu na Maendeleo ya Viwanda, ambapo ilielezwa namna hataza (Ulinzi wa vumbuzi) inaweza kuchochea vumbuzi na maendeleo ya viwanda nchini.

Mikutano hii kwa njia ya video, imeratibiwa na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Video (www.tagla.go.tz), ambapo vituo 7 viliungwanishwa kwenye awamu ya kwanza ya mfululizo wa mikutano hii. Vituo vilivyounganishwa ni pamoja na Dar es Salaam (Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao), Dodoma (TAMISEMI), Kilimanjaro, Kigoma, Lindi, Singida na Pwani.

Mahakama nchini imeendelea kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli zake mbalimbali, ambapo kwa siku mbili mfululizo mashauri tofauti yalisikilizwa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video (Video Conference).

Katika shauri la kwanza, Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara ilisikikila kesi namba 80 ya mwaka 2015 kwa kutumia teknolojia hii, ambapo shahidi muhimu katika shauri hili aliunganishwa kutoka nchini Kanada. Na katika shauri jingine, Mahakama Kuu ilisikiliza kesi ya madai (Civil Case) namba 225 ya mwaka 2013 ambapo shahidi wa kesi hii alikua nchini Uswisi (Switzerland), na mahakama zilihamia kwa muda kwenye kumbi za mikutano kwa njia ya video za Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA). 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti majaji wanaosikiliza kesi hizi wamesema teknolojia hii itawezesha kusikilizwa kwa mashahidi na hatimae kumalizwa kwa mashauri hayo na mengine ambayo ni ya muda mrefu.

 Teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video, ni teknolojia inayowezesha washiriki kutoka vituo viwili au zaidi kuwasiliana kwa kuonana (video) na kusikilizana. Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) imekua ikitoa huduma hizi tangu mwaka 2000 ambapo teknolojia hii imekua ikitumika kwa shughuli mbalimbali kama mikutano ya kawaida, kusikilizwa kwa kesi mbalimbali, usaili, uwasilisho wa miradi na maandiko, midahalo, mafunzo, kuonana na madakrari bingwa, n.k.

Mr. Charles Senkondo, Executive Director of TaGLA during certificate awarding session of Transformational Leadership for Women's Empowerment (TLWE) workshop  organised by TaGLA in collaboration with Skillfocus of Malaysia at TaGLA facilities in Arusha. Mr. Senkondo challenged participants from diverse organisations,  Tanzanian and regional ones to walk the talk, implenting the knowledge of what they have learnt during the workshop by empowering other women. He underpinned the need to empower women in order to tap into the potentials through empowernment of over 50% of the population that are women in attaining family, organisational , national and global economic and social goals.                        

On the right is Ms. Shanta Nagendram, Lead facilitator awarding certificate to Ms. Georgia Edmund who works with TaGLA as an Intern Auditor.

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Zanzibar), Yakout Hassan Yakout na ujumbe wake kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)  wametembelea Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA). Ziara hii ya Katibu Mkuu, inafuatia ziara iliyofanywa na Mkuregenzi Mtendaji na maofisa wengine wa Wakala kwenye taasisi mbalimbali za SMZ.

Lengo la ziara ya Katibu Mkuu, Yakout na ujumbe wake lilikua kujifunza na kujionea shughuli zinazofanywa na Wakala na kuangalia maeneo ya mashirikiano kati ya taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Katibu Mkuu, Bw. Yakout aliongazana na Ndg. Khamis H. Juma (Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu), Ndg. Bakar K. Muhidin  (Mkurugenzi wa Uendeshaji) na Ndg. Shaibu Mwanzema (Mkurugenzi wa Maslahi).

Bw. Yakout alieleza kufurahishwa kwake na huduma zitolewazo na Wakala, hasa huduma za mawasiliano kwa njia ya video, ambapo alisisitiza umuhimu wa huduma hii haswa katika kuleta ufanisi wa utendaji kazi Serikalini na kupunguza matumizi haswa kwenye safari za kikazi na kimasomo. Nae Meneja wa Biashara (TaGLA) alimhakikishia Katibu Mkuu, Yakout kuwa TaGLA kwa kutumia uzoefu wa zaidi ya miaka 16 ilio nao katika maeneo ya mafunzo na teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video imejizatiti kushirikia na SMZ katika maeneo mbalimbali yatakayoamuliwa.

 

Ujumbe kutoka chuo cha Serikali Kenya (Kenya School of Government - KSG) wametembelea Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) kwa nia ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na Wakala katika maeneo ya elimu/ mafunzo kwa njia ya mtandao na teknolojia ya mikutano kwa njia ya video.

Ujumbe huo kutoka Kenya unaongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Dk. Ludeki Chweya,akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao na Maendeleo (eLearning and Development Institute) ya nchini Kenya, Ndg. Joseph Ndungu, iliyoko chini ya mwamvuli wa KSG.

Katika ziara yao ya siku mbili (2 - 3 Februari 2017) hapa nchini, ujumbe huu ulipata nafasi ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakala, lakini pia walipata nafasi ya kutembelea na kufanya mazungumzo na uongozi Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC). Wakuu wa taasisi zote wameona na kusisitiza umuhimu kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya taasisi zao lakini pia kuanzisha maeneo mengine ya kushirikiana kwa manufaa ya taasisi zao na nchi zao kwa ujumla.

Umoja wa Madaktari Bingwa wa Mifupa Duniani (SICOT) ikishirikiana na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), umetoa elimu ya  kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali kwa njia ya mtandao wa mafunzo kwa njia ya video. Umoja huo ulitoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa na wataalamu wa Mifupa kutoka nchi za Tanzania, Marekani, Pakistani na Brazil.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo akiwa TaGLA, Dar es Salaam, Mratibu wa Umoja huo hapa nchini, Dk. Robert Mhina alisema kupitia mafunzo haya wameweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo ajali za barabarani. “Huwa tunajadili mada mbalimbali kama ajali za barabarani kwa kubadilishana uzoefu na Madaktari wa nchi nyingine kwa kutumia mtandao wa mafunzo kwa njia ya video, na wakati wote huwa tunazungumza na nchi kutoka mabara mengine ili kubadilishana uzoefu,”alisema.

Alisema madaktari hao huwa wanakubaliana katika kujadili mada na kujadili kuhusu mambo muhimu yanayohusu tiba ya mifupa huku wakipeana majukumu. “Kupitia vikao hivi hutusaidia sana hata kwa wale wanafunzi wanaojifunza Ubingwa kuona kitu gani kinaendelea duniani, bila gharama za kusafiri nje ya nchi” alisema Dk Mhina.

Alisema tayari Umoja huu inaangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa wanafunzi kutembela vituo kingine katika nchi hizo ili kuona na kuongeza uzoefu zaidi. “Mwaka huu kuna vikao kama sita hivi, kikao hiki ni mwazo tu,”alisema na kuongeza kuwa kupitia mkutano huo itawasaidia wananchi kwa kuboreshewa ufanyaji wa tiba sahihi za mifupa hivyo kupata huduma za matibabu zilizoboreshwa kutokana na ajali za barabarani.

Watoa mada katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video walikuwa ni pamoja na Dk. Syed M. Avais wa King Edward Medical University, Dk. Robert D. Zura MD wa Louisiana State University Health Science Center na Dk. Robert I. Mhina, wa  Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) kutoka nchini Tanzania.

 

 

 

Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) imeingia makubaliano maalumu (MOU) na chuo kikuu ENAP – Canada ili kuweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa Watanzania kwa kutumia teknolojia ya video (Video conferencing). Hatua hii ni muendelezo wa juhudi za Wakala kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo Watanzania wengi zaidi na kwa gharama nafuu.

Kwa kutumia teknolojia hii ya video, Wakala itaweza kuwaleta wataalamu mahiri katika fani za utawala (public administration), usimamizi (management) na uongozi (leadership) kutoka chuo kikuu ENAP kuwasilisha mada kwa washiriki waliopo hapa nchini. Kwa kuanzia TaGLA na ENAP wataendesha kozi  fupi mbili, ambazo ni Project / Program Management: Planning, Monitoring and Controlling, na  “Result Based Management

Ni matumaini ya Wakala kuwa taasisi za Serikali na zile za binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla watatumia fursa hii kukutana na wakufunzi wa kimataifa na kujiongezea ujuzi hatimae kuongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wateja wao. Kozi hizi mbili ni mwanzo tuu, Wakala inatarajia kuendesha mafunzo mengine mengi zaidi kwa kushirikiana na ENAP na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia.