Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

Ujumbe kutoka chuo cha Serikali Kenya (Kenya School of Government - KSG) wametembelea Wakala ya Mafunzo kwa njia ya Mtandao (TaGLA) kwa nia ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na Wakala katika maeneo ya elimu/ mafunzo kwa njia ya mtandao na teknolojia ya mikutano kwa njia ya video.

Ujumbe huo kutoka Kenya unaongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Dk. Ludeki Chweya,akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao na Maendeleo (eLearning and Development Institute) ya nchini Kenya, Ndg. Joseph Ndungu, iliyoko chini ya mwamvuli wa KSG.

Katika ziara yao ya siku mbili (2 - 3 Februari 2017) hapa nchini, ujumbe huu ulipata nafasi ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakala, lakini pia walipata nafasi ya kutembelea na kufanya mazungumzo na uongozi Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC). Wakuu wa taasisi zote wameona na kusisitiza umuhimu kuboresha mahusiano yaliyopo baina ya taasisi zao lakini pia kuanzisha maeneo mengine ya kushirikiana kwa manufaa ya taasisi zao na nchi zao kwa ujumla.

Umoja wa Madaktari Bingwa wa Mifupa Duniani (SICOT) ikishirikiana na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), umetoa elimu ya  kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali kwa njia ya mtandao wa mafunzo kwa njia ya video. Umoja huo ulitoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa na wataalamu wa Mifupa kutoka nchi za Tanzania, Marekani, Pakistani na Brazil.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo akiwa TaGLA, Dar es Salaam, Mratibu wa Umoja huo hapa nchini, Dk. Robert Mhina alisema kupitia mafunzo haya wameweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo ajali za barabarani. “Huwa tunajadili mada mbalimbali kama ajali za barabarani kwa kubadilishana uzoefu na Madaktari wa nchi nyingine kwa kutumia mtandao wa mafunzo kwa njia ya video, na wakati wote huwa tunazungumza na nchi kutoka mabara mengine ili kubadilishana uzoefu,”alisema.

Alisema madaktari hao huwa wanakubaliana katika kujadili mada na kujadili kuhusu mambo muhimu yanayohusu tiba ya mifupa huku wakipeana majukumu. “Kupitia vikao hivi hutusaidia sana hata kwa wale wanafunzi wanaojifunza Ubingwa kuona kitu gani kinaendelea duniani, bila gharama za kusafiri nje ya nchi” alisema Dk Mhina.

Alisema tayari Umoja huu inaangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa wanafunzi kutembela vituo kingine katika nchi hizo ili kuona na kuongeza uzoefu zaidi. “Mwaka huu kuna vikao kama sita hivi, kikao hiki ni mwazo tu,”alisema na kuongeza kuwa kupitia mkutano huo itawasaidia wananchi kwa kuboreshewa ufanyaji wa tiba sahihi za mifupa hivyo kupata huduma za matibabu zilizoboreshwa kutokana na ajali za barabarani.

Watoa mada katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video walikuwa ni pamoja na Dk. Syed M. Avais wa King Edward Medical University, Dk. Robert D. Zura MD wa Louisiana State University Health Science Center na Dk. Robert I. Mhina, wa  Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) kutoka nchini Tanzania.

 

 

 

Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) imeingia makubaliano maalumu (MOU) na chuo kikuu ENAP – Canada ili kuweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa Watanzania kwa kutumia teknolojia ya video (Video conferencing). Hatua hii ni muendelezo wa juhudi za Wakala kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo Watanzania wengi zaidi na kwa gharama nafuu.

Kwa kutumia teknolojia hii ya video, Wakala itaweza kuwaleta wataalamu mahiri katika fani za utawala (public administration), usimamizi (management) na uongozi (leadership) kutoka chuo kikuu ENAP kuwasilisha mada kwa washiriki waliopo hapa nchini. Kwa kuanzia TaGLA na ENAP wataendesha kozi  fupi mbili, ambazo ni Project / Program Management: Planning, Monitoring and Controlling, na  “Result Based Management

Ni matumaini ya Wakala kuwa taasisi za Serikali na zile za binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla watatumia fursa hii kukutana na wakufunzi wa kimataifa na kujiongezea ujuzi hatimae kuongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wateja wao. Kozi hizi mbili ni mwanzo tuu, Wakala inatarajia kuendesha mafunzo mengine mengi zaidi kwa kushirikiana na ENAP na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia.

Board Members have been commended for their role in leading organization during ongoing challenging global situations.

This was said by TaGLA Executive Director Mr. Charles Senkondo during his closing remarks at the end of a course on "Effective Enterprise Risk Oversight". Mr. Senkondo mentioned that we are living in a world of VUCA; a world of Volatility, Uncertainty, Complexity and Ambiguity caused by accelerating globalization and connectivity where Board members are put on the spot. He sighted the September 11, 2001 terrorist attacks in the US where everyone in the world is affected to date, much more impacts are felt on organizations and even on the individual level on the way we relate. He also sighted the Global Financial Crisis that started in the US and has continuously affected the whole world, the developing countries being affected more severely.

Kila tarehe 8 Machi ya kila mwaka Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu, 2016 ni "50  50 ifikapo 2030; Tuongeze jitihada". Kauli mbiu hii inasisitiza kuwa na mikakati madhubuti yenye mwelekeo wa kufikia asilimia 50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja zote za maendeleo.

Kwa kutambua hili, Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao imebuni mafunzo mbalimbali ili kuwajengea wanawake uwezo katika maeneo ya kiuongozi na kiutawala. Kuna mafunzo maalumu kwa ajili ya wanawake mfano; "Transformational Leadership for Women Empowerment" na "Advanced Transformational Leadership for Women Empowerment". Mafunzo mengine ya masuala ya kijinsia ni pamoja na "Gender Based Mainstreaming Workshop".

Wakala pia ina programu mbalimbali katika nyanja nyingine kama manunuzi, TEHAMA, Ugavi na Manunuzi, Usimamizi Rasilimali Watu, n.k. Tembelea tovuti yetu kuweza kujionea programu hizi na huduma nyingine zitolewazo na Wakala.

Baadhi wa maofisa wa ngazi mbalimbali kutoka Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) wameanza mafunzo ya siku 5 ya uandishi na uwasilishaji wa ripoti (Effective Report Writing and Presentation Skills). Mafunzo haya maalum yameandaliwa na TaGLA kwa maofisa hao.

 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora  Mh.Anjela Kairuki (MB), ametembelea Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao ili kujionea kazi za Wakala. Katika ziara hio Waziri Kairuki alipata fursa ya kujionea miuondo mbinu ya wakala, kushiriki katika mkutano wa video na wadau kutoka nchini Kenya, na kisha kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala.

Waziri amewaasa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu ikizingitiwa kuwa Wakala ipo chini ya Ofisi ya Rais.

 

A group photo of participants of the Leadership and Behavioural Change Management workshop which was held from 16th to 23rd June 2014 in Bangalore, India. Participants enjoyed the workshop and arrangements for health checkup at Health Care Global (HCG)