Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

SERIKALI KUANZISHA ZAHANATI ZA BIASHARA

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (VBU) inajipanga kuanzisha Zahanati za Biashara nchini. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Injinia Stella Manyanya wakati wa ufunguzi wa mfululizo wa vikao vya kazi (kwa njia ya Video) kati ya Wizara ya VBU, taasisi zilizopo chini ya Wizara ya VBU na Sekretarieti za Mikoa.

Akifafanua kuhusu Zahanati za Viwanda, Mh. Injinia Manyanya alisema biashara na uwekezaji, kama walivyo binadamu, zinahidaji kuwa na afya ili viweze kuwa na “afya” na kuleta matokeo yaliyotarajiwa. Hivyo Serikali kupitia Wizara, imedhamiria kuona biashara na viwanda vilivyoanzishwa havifi ili kutimiza azma ya Serikali kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Wakati wa Vikao hivyo, Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) iliwasilisha mada kuhusu Milki Ubunifu na Maendeleo ya Viwanda, ambapo ilielezwa namna hataza (Ulinzi wa vumbuzi) inaweza kuchochea vumbuzi na maendeleo ya viwanda nchini.

Mikutano hii kwa njia ya video, imeratibiwa na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Video (www.tagla.go.tz), ambapo vituo 7 viliungwanishwa kwenye awamu ya kwanza ya mfululizo wa mikutano hii. Vituo vilivyounganishwa ni pamoja na Dar es Salaam (Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao), Dodoma (TAMISEMI), Kilimanjaro, Kigoma, Lindi, Singida na Pwani.