Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

TaGLA yang’ara jijini Seoul, Korea Kusini

Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) imewezesha Tanzania kuwa nchi pekee barani Afrika kushiriki Semina za Miji Endelevu zilizoandaliwa kwa kushirikiana na Chuo cha Maendeleo nchini Korea Kusini.

Akitoa taarifa fupi baada ya semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TaGLA Nd. Charles Senkondo alieleza kuwa washiriki 22 kutoka Tanzania walijumuika pamoja na washiriki  zaidi ya 140 kutoka nchi 11 duniani.

 Akiwasilisha mada, Prof. Heungsuk Choi alieleza uzoefu wa nchini Korea Kusini katika kukuza majiji yao kimkakati ili kuweza kuvutia wawekezaji na kuleta maendeleo endelevu ya majiji.

Muendelezo wa semina hizi utakuwepo kwa vipindi vingine sita kati ya sasa na Oktoba 2018, inayofuata imeratibiwa  kufanyika tarehe 26 Juni 2018.

 Nchi zilizoshiriki katika semina hii ni pamoja na China, Vietnam, Philippines, Indonesia, Thailand, Bangladesh, Nepal, Sri Lanka, India, Tanzania na Korea Kusini.

TaGLA ni wakala ya Serikali ya mafunzo kwa njia ya mtandao. Ni moja wapo kati ya mtandao wa vituo zaidi ya 120 duniani (www.gdln.org)

Wito unatolewa kwa watanzania kutumia fursa hii.