Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

TaGLA yafungua warsha ya mafunzo ya mfumo wa wazi wa ukaguzi na utathmini (OPRAS) jijini Tanga.

Wakala ya mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) yafungua warsha ya siku tano ya mafunzo ya mfumo wa wazi wa ukaguzi na utathmini (OPRAS)  jijini Tanga. Warsha hiyo ya siku tano inashirikisha washiriki 16 baada ya warsha hiyo washiriki watakabidhiwa vyeti vya ushiriki.

TaGLA ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245 ikiwa na jukumu la kujenga uwezo wa watumishi wa umma na sekta binafsi kwa kutumia teknolojia na njia bunifu. Pia ni mwanachama wa Chama cha Vituo vya Mafunzo ya Maendeleo barani Afrika (AADLC) na Mtandao wa Mafunzo ya Maendeleo Duniani (GDLN) vyenye jukumu la kuwezesha watoa maamuzi na wataalamu pamoja na watendaji kupata na kushirikishana uzoefu na ujuzi uliopo duniani .

TaGLA inatoa wito kwa wadau mbalimbali kutembelea tovuti yetu ya www.tagla.go.tz ili kujua mafunzo na huduma mbalimbali zitolewazo na wakala.