Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

TaGLA yatoa ya mafunzo ya Matumizi Bora ya Mifumo ya Mawasiliano kwa Njia ya Video (Video Conference)

Wakala ya mafunzo kwa njia ya mtandao (TaGLA) imetoa mafunzo ya matumizi bora ya Mifumo ya Mawasiliano kwa Njia ya Video ikilenga kuongeza ufanisi katika utendaji kwa kutumia TEHAMA.

Akifungua mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa TaGLA Ndg Charles Senkondo alisema mafunzo hayo ni ya kuwapa uwezo waandaji wa mafunzo, walengwa wa mafunzo na wana TEHAMA wanaowezesha mifumo ya mawasiliano kwa njia ya video.

Akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo, Meneja TEHAMA wa Wakala Nd. Emmanuel Tessuaa alieleza faida za matumizi ya teknolojia hii ni pamoja na kuokoa muda, kupunguza gharama na usumbufu wa safari, kufikia walengwa wengi kwa wakati mmoja, kufikia maamuzi ndani ya muda mfupi, nk.

Alitoa wito kujiunga na mafunzo hayo ya siku moja ili kupata uelewa wa matumizi bora ya teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video (video conference) ili kuongeza ufanisi katika utendaji.

TaGLA ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245 ikiwa na jukumu la kujenga uwezo wa watumishi wa umma na sekta binafsi kwa kutumia teknolojia na njia bunifu. Pia ni mwanachama wa Chama cha Vituo vya Mafunzo ya Maendeleo barani Afrika (AADLC) na Mtandao wa Mafunzo ya Maendeleo Duniani (GDLN) vyenye jukumu la kuwezesha watoa maamuzi na wataalamu pamoja na watendaji kupata na kushirikishana uzoefu na ujuzi uliopo duniani .

TaGLA inatoa wito kwa wadau mbalimbali kutembelea tovuti yetu ya www.tagla.go.tz ili kujua mafunzo na huduma mbalimbali zitolewazo na wakala.