Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

TaGLA KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI ZA CONTINENTAL-INDIA WAENDESHA MDAHALO WA "PLASTIC SURGERY AND RECONSTRUCTION"

Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) kwa kushirikiana na Hospitali za Continetal India, wamefanya Mdahalo wa Kitaaluma kwa njia ya video (videoconference) kuhusu Upasuaji kwa ajili ya Kurekebisha Maumbile na Urembo (Plastic Surgery and Reconstruction).  Mdahalo huo uliendeshwa na Daktari Rajeshi Vasu ambaye ni Bingwa wa Upasuaji wa kurekebisha  mwili na Urembo ambaye pia ni Mkuu wa idara hiyo katika hosiptali za Continental nchini India.

Washiriki wakiwa TaGLA, Dar es Salaam walikuwa Madaktari, Wasomi, Kampuni za Bima za Afya na wanataaluma ambao waliomba kuwepo na muendelezo ili kupata ufahamu zaidi juu ya huduma hizo muhimu. Kwa maelezo zaidi https://youtube.be/Hmo7xiDvB_w