Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

USIMAMIZI WA MITIHANI

Elimu ya masafa na mafunzo kwa njia ya mtandao ni mtindo mpya wa elimu duniani. Kutokana na mahitaji ya kikazi, mahitaji ya kukaa na familia na majukumu mengine huwakwamisha watu wengi kusafiri kwenda kusoma darasani. Teknolojia imewasaidia watu kusoma popote walipo, wakati wowote.

Usimamizi wa mitihani ya mtandaoni haipaswi kuwa tatizo tena kwani TaGLA inatoa huduma ya usimamizi wa mitihani kwa wanaofanya mitihani ya aina hii. Sisi ni kituo cha mitihani cha kuaminika kimataifa, na ni wasimamizi mahiri wa mitihani.

 TaGLA tuna uhakika na;

  • Mazingira tulivu na mazuri kwa mitihani,
  • Wasimamizi wa mitihani mahiri, wenye weledi na waliothibitishwa, 
  • Kuna intaneti,nukushi nzuri na mtandao wa uhakika kwa ajili ya kutuma na kupokea mitihani,
  • Kuna jenereta wakati wote,
  • Tunapatikana kwa saa 24 kwa siku 7.