Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

HUDUMA ZA MIKUTANO KWA NJIA YA VIDEO

Teknolojia ya Mikutano kwa Njia ya Video husaidia kuendesha mikutano miwili au zaidi kwa wakati mmoja na huwawezesha washiriki kuwasiliana kupitia video na kusikia sauti.TaGLA, ambayo inaongoza nchini Tanzania kwa kutoa huduma za mikutano kwa njia ya video, tuna uzoefu wa zaidi ya miaka kumi na tano (15) na tuna wataalamu wa kutosha katika uwanja huu, na hivyo tanafahamu kuifanya teknolojia hii kuwa rahisi kuitumia. Kutokana na uzoefu wetu, tunaweza kuandaa na kuratibu shughuli za mikutano kwa njia ya video katika mji wowote duniani. Pia tuna uwezo wa kuunganisha mifumo/maeneo ya mikutano video zaidi ya mawili kwa wakati mmoja. Aidha, tunaweza kuunganisha mifumo ya video iliyo katika IP na ile ya ISDN.  

Huduma hizi zina manufaa gani kwako?

Vyumba vyetu vyenye huduma ya Mikutano kwa Njia ya Video vinaweza kutumika kwa ajili ya:

 • Meetings 
 • Mikutano
 • UsailiMafunzo
 • Kuendesha Kesi
 • Huduma za Matibabu
 • Uwasilishaji (Miradi, mawasilisho ya kitaaluma, n.k)
 • Majadiliano mbalimbali /li>
 • Warsha na Semina
 • Shughuli nyingine yoyote ilmradi kuna intaneti na taknolojia inayohitajika katika eneo hilo.

Ni nzuri kama vile uko pale

Fanya uamuzi sahihi na kwa wakati. Kutana na mtu yeyote, popote na kwa wakati wowote. 

 • Okoa fedha isipotee kwa kusafiri na malazi
 • Epuka kujitaabisha kwa kutembea kwa miguu
 • Jiunge na kituo kimoja au zaidi ya vituo 1,200 duniani
 • Fanya maombi yako mapema, kwa njia rahisi na kwa gharama nafuu

Yeyote aliyejaribu kushiriki kamwe hajajuta, wamekuwa wadau wa kila siku, je unataka kujua siri ya mafanikio? Fanya maombi yako mtandaoni sasa au zungumza na Meneja wetu wa Masuala ya Kiutawala kupitia simu nambari +255 222 123705/09.

.........Karibu sana TaGLA kwa huduma bora za mikutano kwa njia ya video..........