Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

HUDUMA ZA VIFAA VYA MAWASILIANO YA KITEKNOLOJIA

UkiwaTaGLA utapata vifaa anuwai vya mawasiliano kiteknolojia ikiwa ni pamoja na projekta, compyuta zilizounganishwa kwenye mkongo wa mawasiliano ya Intaneti. Kuna maabara mbili za vifaa anuwai vya mawasiliano, moja ina kompyuta 30 (Chumba cha Kilimanjaro cha Vifaa vya Mawasiliano ya Kiteknolojia) na nyingine ina kompyuta 18 (Chumba cha Mikumi cha Vifaa vya Mawasiliano ya Kiteknolojia). Hata hivyo, tuna kompyuta pakatwa (laptops) ambazo zinaweza kuunganishwa popote kwenye vyumba vyetu na kwenye maeneo ya wateja wetu pale inapohitajika.

Chati mgeuzo, kalamu, video, ubao mweupe na kalamu za kuandikia hutolewa kama sehemu ya gharama za ukumbi huu.. Huduma ya chai, kahawa,vitafunwa na chakula cha mchana au jioni inaweza kutolewa kama mteja atahitaji huduma hizo

  • Vifaa vya kufanyia mawasilisho vilivyounganishwa na kompyuta au kompyuta pakatwa
  • Teknolojia ya kutuma data nyingi kwa kasi
  • Ubao mweupe/chati mgeuzo na kalamu
  • Viburudisho
  • Viti 50, 30, 20 na 8 kwa mkao wa mhadhara

.........Karibu sana TaGLA kwa huduma bora za vifaa vya mawasiliano ya kiteknolojia ..........