Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

Vestibulum id urna

Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245 ikiwa na jukumu la kujenga uwezo wa watumishi wa umma na sekta binafsi kwa kutumia teknolojia.

TaGLA ni mwanachama wa Chama cha Vituo vya Mafunzo ya Maendeleo barani Afrika (AADLC) na Mtandao wa Mafunzo ya Maendeleo Duniani (GDLN) ambao una mtandao wa vituo 120 vya taarifa za maendeleo duniani. AADLC na GDLN vina jukumu la kuwezesha watoa maamuzi na wataalamu pamoja na watendaji wa ngazi ya kati kupata na kushirikishana uzoefu na ujuzi uliopo duniani kupitia mifumo ya mawasiliano kwa njia ya mtandao ikiwa ni pamoja na mikutano kwa njia ya video, intaneti, video, CD-ROM, na machapisho mbalimbali.

TaGLA ni chombo cha umma, siyo chombo cha kutengeneza faida, ambacho kwa baadae kitakidhi mahitaji yake kutokana na mapato kinayozalisha. Kwa mantiki hiyo, Wakala utaendeshwa kwa kuzingatia maslahi ya umma pamoja na uchanganuzi wa faida na hasara.

Dira Yetu

Kuwa kituo cha pekee duniani cha kuzalisha, kuhawilisha na kushirikishana maarifa na ujuzi.

 

Dhamira Yetu

Kujenga uwezo kupitia programu maalum za mafunzo ya maendeleo duniani na midahalo ya kushirikishana maarifa na ujuzi kwa njia za kiteknolojia kwa lengo la kutoa huduma bora.

 

Maadili Yetu ya Msingi

TaGLA unatekeleza mambo makuu matano ambayo yanaonyesha majukumu yetu makuu, nayo ni:

•Kujielekeza kwa wateja

•Kufanya vizuri zaidi katika huduma

•Uadilifu

•Kujituma kwenye kazi

•Ubunifu