Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

Kupanga Kustaafu - Kujiandaa Maisha baada ya kustaafu

Utangulizi

Kituo cha Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (Tanzania Global Learning Centre (TaGLC) imeandaa mafunzo ya Kujiandaa na Maisha Baada ya Kustaafu Kazi. Mafunzo haya ni fursa ya pekee kwa wafanyakazi walio katika ajira rasmi kuweza kutafakari,kutathimini na kupanga maisha yao baada ya kustaafu. Mafunzo haya yataendeshwa kwa muda wa siku tano .

 

LENGO

Lengo la mafunzo haya ni kuwapa washiriki maarifa,mbinu na uzoefu wa jinsi ya kujiandaa vema na maisha baada ya kustaafu. Tafiti mbalimbali zimebaini kuwa wastaafu wengi hukumbwa na  misukosuko mingi ya kifedha, kiafya na kimaisha kwa ujumla. Moja kati ya sababu kubwa  ya wastaafu kukumbwa na misukosuko hiyo na kushindwa kuihimili vema ni kutokuwa na mipango madhubuti ya maisha baada ya kustaafu kazi.

Mafunzo ya Kujiandaa na Maisha Baada ya Kustaafu Kazi   yamelenga     kumwezesha mfanyakazi kuanza mapema kuandaa mpango binafsi wa kujiandaa kustaafu.   Mafunzo pia yatatoa fursa  kwa washiriki                  kubadilishana ufahamu na uzoefu     kutokana na  mazingira watokayo.

 

Malengo mahsusi ya mafunzo haya ni:-

· Kuwaandaa washiriki kisaikolojia juu ya maisha baada ya kustaafu,

· Kuwaelimisha juu ya kuandaa mpango binafsi wa kustaafu,

· Kuwapa mbinu za kijasiriamali na stadi za maisha,

· Kutoa elimu ya afya.

 

 WALENGWA

Wale wote walio   katika ajira rasmi.

 

 Tarehe:  4– 8 Mei 2020 Mahali : Morogoro

 

Course Properties

Course date: 04-05-2020 8:00 am
Course End Date: 08-05-2020 4:00 pm
Capacity Unlimited
Location Morogoro