Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

Hiki ni chumba ambacho kipo ghorofa ya chini. Chumba hiki hutumika kwa ajili ya mahojiano kwa njia ya video, mikutano ya biashara, semina na warsha, mafunzo na mikutano ya kawaida na kina uwezo wa kukaa watu hadi 30 kwa wakati mmoja. Vifaa vyote ikiwamo projekta, intaneti, chati mgeuzo, ubao, n.k. vimo katika chumba hiki.

Maabara hii ipo ghorofa ya kwanza na inatumika kwa ajili ya mafunzo mbalimbali ya kikompyuta. Maabara ya Mikumi ina uwezo wa kuchukua washiriki hadi 20 kwa wakati mmoja. Maabara hii ina vyombo vyote muhimu vya mafunzo yanayohitaji vifaa muhimu vya mawasiliano ya kiteknolojia na mafunzo ya kikompyuta. Miunganisho iliyopo na upatikanaji wa mtandao wa data ya kielektroniki ya wadau vipo katika chumba hiki, hali inayoruhusu upatikanaji na utoaji wa mafunzo kuhusu mifumo mbalimbali ya taarifa iliyopo kwenye ofisi za wadau na intaneti.

Maabara ipo ghorofa ya saba na kinatumika kwa ajili ya mafunzo mbalimbali ya kikompyuta. Maabara hii inaweza kuchukua watu 30. Maabara ya Kilimanjaro imesheheni kila aina ya vifaa muhimu kwa ajili ya mawasiliano ya kiteknolojia na mafunzo ya kikompyuta. Miunganisho iliyopo na upatikanaji wa mtandao wa data ya kielektroniki ya wadau vinasaidia katika ufundishaji wa mifumo mbalimba ya taarifa iliyopo katika ofisi za wadau na kwenye intaneti.

Chumba hiki kipo ghorofa ya saba (7) na kinatumika kwa ajili ya mikutano kwa njia ya video na mambo mengine kama vile mikutano, warsha na mafunzo ya ana kwa ana. Kina uwezo wa kuchukua washiriki hadi 50. Chumba hiki kina vifaa vya kisasa vya mikutano kwa njia ya video, projekta na kina skrini kubwa Zenye uwezo wa kuonyesha washiriki walio mbali kwa uhalisia wao. Pia kuna mitambo ya kudhibiti joto, mwanga na sauti za washiriki.  

Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao una Kituo cha Taarifa za Maendeleo kinachomilikiwa na wabia mbalimbali, ambacho kinajulikana kwa Kiingereza kama ‘The Tanzania Development Information Center – TDIC’. TDIC ni kituo muhimu kwa ajili ya kupata taarifa za maendeleo kutoka kwa wadau mbalimbali wanaowasilisha taarifa zao na hivyo, kinasaidia upatikanaji wa taarifa hizo katika kituo kimoja. 

Hiki ni chumba kizuri chenye ubora wa hali ya juu ambacho kipo ghorofa ya kwanza. Chumba hiki kina uwezo wa kuingiza watu 10 kwa wakati mmoja. Katika chumba hiki kuna Projekta, Intaneti Isowaya (WiFi), kiyoyozi, jenereta na vifaa vingine muhimu.