Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

TaGLA yaingia Makubaliano na Chuo Kikuu cha ENAP – Canada

Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) imeingia makubaliano maalumu (MOU) na chuo kikuu ENAP – Canada ili kuweza kutoa mafunzo mbalimbali kwa Watanzania kwa kutumia teknolojia ya video (Video conferencing). Hatua hii ni muendelezo wa juhudi za Wakala kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo Watanzania wengi zaidi na kwa gharama nafuu.

Kwa kutumia teknolojia hii ya video, Wakala itaweza kuwaleta wataalamu mahiri katika fani za utawala (public administration), usimamizi (management) na uongozi (leadership) kutoka chuo kikuu ENAP kuwasilisha mada kwa washiriki waliopo hapa nchini. Kwa kuanzia TaGLA na ENAP wataendesha kozi  fupi mbili, ambazo ni Project / Program Management: Planning, Monitoring and Controlling, na  “Result Based Management

Ni matumaini ya Wakala kuwa taasisi za Serikali na zile za binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla watatumia fursa hii kukutana na wakufunzi wa kimataifa na kujiongezea ujuzi hatimae kuongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wateja wao. Kozi hizi mbili ni mwanzo tuu, Wakala inatarajia kuendesha mafunzo mengine mengi zaidi kwa kushirikiana na ENAP na vyuo vingine vya ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia.

 

Kuhusu TaGLA

Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Sura ya 245 ikiwa na jukumu la kuwawezesha wananchi kupata, kushiriki na kuwezesha upatikanaji wa elimu pamoja na kutafakari  juu ya ajenda ya maendeleo ya kimataifa kwa njia ya teknolojia.

Dira

Kuwa kituo cha pekee duniani cha kuzalisha, kuhawilisha na kushirikishana maarifa na ujuzi.

Dhamira

Kujenga uwezo kupitia programu maalum za mafunzo ya maendeleo duniani na midahalo ya kushirikishana maarifa na ujuzi kwa njia za kiteknolojia kwa lengo la kutoa huduma bora.

Kuhusu ENAP

Ecole nationale d’administration publique (ENAP) ni moja kati ya vyuo vikuu vikubwa vya utawala wa umma (Public Administration) duniani. Chuo hichi kilianziswa mwaka 1969, na tangu kipindi hicho kimekuwa mstari wa mbele katika kuhuisha utawala wa umma wa kisasa na ufanisi ndani ya Canada na duniani kwa ujumla. Soma zaidi kuhusu ENAP hapa