Wasiliana Nasi: info@tagla.go.tz | +255 22 2123705 / +255 22 2123709 / +255 22 223711

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Zanzibar Atembelea TaGLA

 

Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Zanzibar), Yakout Hassan Yakout na ujumbe wake kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)  wametembelea Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA). Ziara hii ya Katibu Mkuu, inafuatia ziara iliyofanywa na Mkuregenzi Mtendaji na maofisa wengine wa Wakala kwenye taasisi mbalimbali za SMZ.

Lengo la ziara ya Katibu Mkuu, Yakout na ujumbe wake lilikua kujifunza na kujionea shughuli zinazofanywa na Wakala na kuangalia maeneo ya mashirikiano kati ya taasisi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Katibu Mkuu, Bw. Yakout aliongazana na Ndg. Khamis H. Juma (Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu), Ndg. Bakar K. Muhidin  (Mkurugenzi wa Uendeshaji) na Ndg. Shaibu Mwanzema (Mkurugenzi wa Maslahi).

Bw. Yakout alieleza kufurahishwa kwake na huduma zitolewazo na Wakala, hasa huduma za mawasiliano kwa njia ya video, ambapo alisisitiza umuhimu wa huduma hii haswa katika kuleta ufanisi wa utendaji kazi Serikalini na kupunguza matumizi haswa kwenye safari za kikazi na kimasomo. Nae Meneja wa Biashara (TaGLA) alimhakikishia Katibu Mkuu, Yakout kuwa TaGLA kwa kutumia uzoefu wa zaidi ya miaka 16 ilio nao katika maeneo ya mafunzo na teknolojia ya mawasiliano kwa njia ya video imejizatiti kushirikia na SMZ katika maeneo mbalimbali yatakayoamuliwa.